Kwenye
uzinduzi wa chibu perfume Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK
alitangaza bei ya Perfume ya Chibu itakavyouzwa kwenye maduka, baadhi
ya watu wamesema kuwa bei hiyo ni kubwa sana,ndipo “Diamond
Platnumzi” akaamua kufunguka kwa kusema haya;
"Diamond
anatambua kuwa ili kusonga mbele mtu anapaswa kujitoa katika
kutengeneza kitu au bidhaa yenye ubora”,
"pia
amesema kwa sasa chibu perfume imeingia kwenye chupa ya ujazo wa
ml100 kama bidhaa ya kuanzia lakini kwa baadae watatengeneza kwa
vipimo tofautitofauti ili wadau mbalimbali wenye uzalendo na
wanaoweza kusapoti kazi za wazalendo waweze kunufaika na huduma toka
kwa wazalendo wenzao”.
:"Amesisitiza
vijana kuendelea kuwa wabunifu,serikali itoe mchango wake kwa
kuwasapoti vijana wao na kuonesha njia kwa vijana wengine kuwa
inawezekana,kufanya kitu na kuleta ushinadani kwenye masoko makubwa
kidunia.”
"Aliongeza kwa kusema gharama za uzalishaji wa bidhaa hiyo ilikuwa juu,kutokana na ubora wa bidhaa ambayo inahitajika sokoni,na uhitaji wa kukamata soko la ushindani,na anatambua mchango wa wadau tofauti katika kufikia malengo,kama media zote,watanzania na anaamini huu ndio mwanzo na muendelezo wa kuanzishwa kwa bidhaa nyingine zitakazobuniwa na vijana wa kitanzania".
No comments:
Post a Comment