Leo
Septemba22, 2017 mechi ya pili ya mashindano ya Ndondo Cup Mwanza
imechezwa kwenye uwanja wa Nyamagana ikizikutanisha Iseni FC vs Copco
FC amba timu hizo zimetoka sare ya kufungana magoli 2-2.
Copco
walitangulia kufunga magoli yote mawili kipindi cha kwanza, Kisandu
Faustine alifunga bao la kwanza dakika ya 16 kisha David Brand
akafunga bao la pili dakika ya 35 na kuendelea kuiweka timu yake
mbele kwa magoli 2-0 ndani ya kipindi cha kwanza.
Kipindi
cha pili Iseni walipambana kuhakikisha wanasawazisha magoli hayo,
Hatibu Abdallah akaifungia Iseni magoli yote mawili kipindi na
kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 2-2
No comments:
Post a Comment