Maandamano
makubwa yajiri nchini Morocco ambapo mamia ya walioandamana
wameonekana katika mitaa kadhaa maarufu kwenye mji mkuu wa nchi hiyo
Rabat, huku kundi kubwa la waandamanaji likishamiri eneo la Kaskazini
mwa nchi hiyo.
Hali
ya sintofahamu imeendelea kuonekana ,huku wasi wasi ulioletwa na
vurugu nje ya mji wa al-Hoceima,ambapo ilisemekana polisi walijaribu
kumshikilia mwanaharakati maarufu Nasser Zefzafi anayedaiwa kuhusika
katika kuvuruga ibada kwenye moja ya msikiti.
Hali
ya maandamano ilionekana kushamiri tangu mwezi Oktoba mwaka jana
baada ya mfanyabiashara maarufu wa samaki al-Hoceima aliyeuawa wakati
akiwazuia maofisa wa serikali wasiharibu ghala la samaki wake.
No comments:
Post a Comment