Mchezaji wa Simba SC, Jonas Mkude anaendelea vizuri akiwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako amefanyiwa vipimo
na kupata matibabu baada ya kupata ajali
ya gari. kwenye ajali hiyo mtu mmoja
ambaye pia inasemekana ni shabiki mkubwa wa “Simba“Shose
Fidelis amepoteza maisha.
Ajali ambayo ilitokea siku moja tu baada ya Mkude kuiongoza
Simba kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma,Kiungo huyo alifikishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ili kupata uhakika
wa afya yake.
Lakini hali yake imeendelea kuimarika na ijapokuwa jana alikuwa akilalama
sana maumivu lakini sasa ana nafuu.
No comments:
Post a Comment